HISTORIA YA MADILU SYSTEM

0:00

Amezaliwa:28 Mei 1952

Amekufa:11 Agosti 2007

Jean de Dieu Makiese kama wengi tumjuavyo Madilu System, alikuwa mwimbaji wa Sokous na Mtunzi aliezaliwa Leopoldville ,Belgia Congo. Ni mmoja ya waimbaji kwenye kundi la TP OK Jazz ambayo ilitamba sana miaka ya 1960,1970 na 80.

Alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 19 hapo Kinshasa tokea mwaka wa 1971. Kwenye umri wa miaka 15 alikuwa akiimba na Orchestre Symba,Papa Noel na Orchestra Bambula ya Sam Mangwana na baadae bendi yake ya Orchestra Baku Bakuba Mayopi lakini pamoja na kuwa Kwenye majukwaa hakuna aliemfahamu. Ni Franco aliemfanya kuwa nyota na kumpa jina la Madilu System. “Mamou (Tu vois), ni kibao kilichotambulisha nyota mpya kwenye kundi la T.P . OK Jazz mnamo mwaka 1984. Baada ya wimbo huo, Madilu System nae akaja na wimbo wake wa “pesa Position “ na baadae “Mario” na “Reponse de Mario” mwaka 1985 na pia moja ya kolabo bora ni ya “La Vie des Hommes” ya mwaka 1986.

🇨🇩 huenda ina waimbaji wazuri sana kuliko Madilu,ila waliojaribu kuiga kwenye mipangilio ya Madilu ya uimbaji walifeli vibaya mno. Kwa u ubora wa uimbaji wake ndio maana hata Franco alimuelewa haraka. Ushahidi wa hiki ni kwenye nyimbo nyingi za Franco ambazo alimtumia Madilu kama mtu ambaye wanajibizana,kwakweli waliendana.

Wakati Franco anafariki mwaka 1989,T.P.O.K Jazz ilimpa heshima kwa kuacha kutumbuiza kwa mwaka mmoja lakini baadae walirudi na Madilu akiwa miongoni mwa viongozi. Kwa kipindi hicho ambacho Franco hakuwepo alihakikisha ustawi wa bendi upo huku nae akianza tena shughuli za mziki wake binafsi nje ya kundi. Kiukweli kwenye solo nje ya Sam Mangwana hakuna mkongwe mwingine aliemfikia Madilu. Pamoja na Madilu kuamua kuishi zake Uswizi na ufaransa kamwe hakupungukiwa na mashabiki kwenye nchi yake ya Congo. Bado aliposhirikishwa kwenye nyimbo mfano na Nyboma Mwandido na Josky Kiambukuta alifanya balaa kubwa.

See also  MFAHAMU BALOZI ALI IDI SIWA MKURUGENZI MPYA USALAMA WA TAIFA

Mwaka 2006 aliachia Albamu mpya ya “La Bonne Humeur”,ilikuwa ni album iliofanya vizuri hasa ikizingatiwa kumbe ndio ilikuwa Album yake ya mwisho. Alikwenda Kinshasa mwanzoni mwa mwezi August akiwa kwenye kurekodi video alianguka na ilikuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 10 na baadae alikimbizwa hospital ya chuo kimoja na asubuhi yake Madilu System aliaga Dunia.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Utata vifo vya watu 11 kiwanda cha...
HABARI KUU Watu 11 wakiwemo raia watatu kigeni wamefariki dunia...
Read more
STAN BOWLES AFARIKI DUNIA
HABARI KUU Nyota wa zamani wa QPR, Manchester City na...
Read more
Grim Discovery at Kware Dumpsite Sparks Calls...
The Governor of Siaya County, James Orengo, has called on...
Read more
Historia ya Mwanamziki Diamond platnumz
Nasibu Abdul Juma Isaac (maarufu kwa jina la kisanii kama...
Read more
NAFASI YA UENEZI INAVYOITESA CCM ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply