Dar es salaam
Kupitia kwa Wakili Eric S Ng’maryo , Rais wa Zamani wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Abdullahman Kinana wamepanga kumshitaki Mhariri wa Gazeti la Mwanahalisi ndg Said Kubenea kwa kile kinachotajwa ni kuwasingizia kwenye chapisho Lake kuhusu wao kuwa vinara wa kupinga Mkataba wa Uwekezaji kati ya Bandari ya Dar es salaam na DP WORLD.
Wakili huyo amesisitiza kwa kumtaka Kubenea kuomba msamaha ndani ya siku 14 na iwapo hatotii basi watamfungulia mashtaka kwa kuwazalilisha.
Aidha, kwa siku za karibuni sakata la Bandari limechukua vichwa vya habari kuhusu Mkataba wa awali wa Uwekezaji kuwa na mapungufu mengi ya kisheria ambayo yameonekana yatakuwa mwiba kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Baadhi ya watu waliionekana kuupinga Mkataba wa Uwekezaji ukiacha vyama kama CHADEMA ni pamoja na Waziri wa Zamani wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge Mstaafu Jimbo la Muleba Kusini Mh Anna Tibaijuka.
Kwenye gazeti hili la Mwanahalisi ,limeweka wazi kuwa Kinana na Kikwete wanaupinga Mkataba huu kwasababu wangependelea serikali ibaki na TICTS ambayo kipindi cha Awamu ya Tano,chini ya Rais John Pombe Magufuli walikataliwa kuongezewa muda zaidi wa Uwekezaji mpaka unaisha mwaka huu 2023. Pamoja na hayo ,inatajwa nyuma ya hakina Kikwete na Kinana wapo hakina Nazir Mustaafa Karamagi boss huyu wa Zamani wa TICTS na makampuni makubwa kama GSM ambayo inadaiwa wao ni wanufaika wa Bandari.
Serikali ililenga kuweka mwekezaji mpya kwa kile walichosema wamekuwa wakipoteza bilioni zaidi ya 100 kila Mwezi kwenye Bandari ya Dar es salaam.