<!--INDOLEADS - BEGIN-->
Makala Fupi
Ni MUNGU tu mwenye Mamlaka ya kumruzuku kiumbe wake riziki katika Mazingira yoyote yale, ni MUNGU ambaye anaweza kukupitisha kwenye changamoto hili akupe pumziko jema. Kwenye vitabu vya Dini tunaambiwa ,kuna watu walistahili kuingizwa motoni yaani Jehanam lakini kwa neema na rehema za Mwenyezi MUNGU yeye atawaandalia njia wao wapone adhabu hiyo kwa kupitia watu wengine mathalani watu wanaouwawa bila ya sababu.
Ni kinda BERNARD KAMUNGO aliezaliwa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Kigoma ,Tanzania ambaye kwa hivi sasa ni Nyota wa Mpira kwenye klabu ya Dallas Fc. Ndoto yake kamwe haikuwa mpira lakini amefika hapo baada ya Wazazi wake kuokolewa kwa kupelekwa Nchini Marekani wakiwa ni wakimbizi .
BERNARD anasema “niliacha shule nikiwa na umri wa miaka 11 ,nikiwa darasa la Nne hili niweze kuisaidia Familia yangu”. Ndoto ya kucheza kambumbu kwa kinda huyu ilianza baada ya kuamia Marekani kwenye timu ya North Texas SC ambapo kwenye michezo 7 alipachika goli 1.
Hivi karibuni Bernard Kamungo alikuwa nyota baada ya kupachika goli dhidi ya timu ya Lionel Messi gwiji wa soka Duniani Inter Miami kwenye Michuano ya North and Central America League Cup, ambapo walitoka kwa sare ya 4-4 na baadae mikwaju ya penati ndio iliwapa ushindi Inter Miami wa jumla ya 5 kwa 3. KAMUNGO, amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza dhidi ya nguli Leo Messi.