London,Uingereza.
Timu ya Manchester City imeendeleza pale ilipoishia kwenye msimu wa 2022-23 leo baada ya kuichapa timu ya Burnley kwenye ufunguzi wa msimu wa 2023-24.
Ilikuwa ni dakika ya 4 ya mchezo,ambapo Mnorwei Erling Haaland alipachika bao lake la kwanza na kwa Manchester City na pia Ligi nzima likiwa ndilo goli la ufunguzi wa pazia la Ligi kuu ya England akipokea pasi ya mwisho ya Julian Alvarez. Dakika ya 36 kabla ya Mapumziko ,Manchester City imefanikiwa kupata goli la pili kupitia kwa yuleyule Erling Haaland akifunga pasi ya Rodri na baadae Rodri dakika ya 75 amefunga goli la tatu na kuhitimisha kalamu hiyo ya ushindi kwa Manchester City iliopo chini ya Mkufunzi Pep Guardiola.
Mchezo wa leo umeanza vibaya kwa timu ya Burnley ni baada ya Mlinzi wao Anass Zaroury kutolewa kwenye dakika za nyongeza za Mchezo kwa kadi nyekundu huku pia nayo Manchester City ikimpoteza Kelvin Debryun ametolewa kwa majeraha na nafasi yake ikichukuliwa na Mateo Kovacic.
Aidha, katika mchezo wa leo kulitokea shabiki aliempiga mchezaji wa Burnley ambapo kupitia Mamlaka za uwanja wa Burnley inatajwa mtu huyo amekamatwa kwa hivi sasa.