Makala Fupi
Maisha halisi ya Mwanamke anayetarajia kuwa mke kwa maana ya maandalizi au mwenendo yana mambo yafuatayo;
UVUMILIVU
Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbalimbali yasiyovutia katika maisha/mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama Mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile chuki,kulaumu,ugomvi,vurugu,malalamiko,manung’uniko,machado,kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako .Hivyo Mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo.
UPENDO WA DHATI
Maisha ya Upendo wa halisi na sio wa kinafiki kwa jamii inayomzunguka . Tabia ya Upendo halisi ina thamani kubwa sana kuliko Mali nyingi,pesa,elimu ya juu nk wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo Upendo halisi ni sawa na bure, Nguzo kuu ya maisha ya Mwanamke shujaa ni Upendo wa dhati na uhalisia.
UTII KWA JAMII
Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupitia kona yoyote. Utii kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama Mwanamke.
UAMINIFU KATIKA JAMII
Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa pekee aweze kutunza uaminifu kwa jamii inayomzunguka. Mwanamke hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika nyanja zote.
UNYENYEKEVU WA KWELI.
Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi majivuno,kujigamba,kujikweza,kujiinua,kujiona,na hata kujitanguliza mbele kwa kila jambo.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.