JE TIMU YA CHELSEA INAENDA KUTAWALA SOKA ?

0:00

Klabu ya Chelsea ya Magharibi mwa London imemtangaza mchezaji Moises Caicedo (21) ambae alikuwa mchezaji muhimu kunako kikosi cha Brighton & Hove Albion msimu wa 2022-23.

Chelsea wamelipa jumla ya Euro milioni 115 ambayo ni Euro milioni 5 zaidi ya ofa ya klabu ya Liverpool na Moises Caicedo atacheza klabuni hapo kwa miaka 08 mtawalia na akiwa na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka 01. Fedha hii ni kubwa na ni rekodi ambayo inawekwa na Chelsea hiyo hiyo ambayo hivi karibuni ilimsajili kiungo Enzo Fernández kwa Euro 106. Kwa fedha hizi ni dhahiri Chelsea ina timu ghali zaidi kwasababu hawa viungo wana thamani ya Euro 221.

Usajili huu wa Chelsea ni kama kwa upande mmoja umewaua Liverpool nguvu kwasababu ya kwamba nae alihitaji huduma ya hawa viungo ,inatajwa Liverpool walipewa nafasi na klabu ya River Plate ya Argentina ya kumsajili kiungo wa Chelsea Enzo Fernández kipindi kilichopita cha usajili cha majira ya joto kwa dau la Euro milioni 15 kabla hajasajiliwa na klabu ya Benifica ya nchini Ureno kwa dau la Euro milioni 44.24

Baada ya usajili huu ,nguli Michael Owen ametia neno akisema Chelsea wanakwenda kuwa na kiungo imara zaidi kwenye ligi ya soka nchini Uingereza na akitabiri kuwapiku Manchester City ya Kelvin De Bryun.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  YANGA NA SIMBA KUKUTANA APRIL 20
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading