Johannesburg
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ni kuwa kundi la Mataifa yanayoibuka kiuchumi (BRICS), Januari 2024 litapokea Wanachama wapya ambao ni Argentina, Misri, Ethiopia, Iran,Saudia Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Ramaphosa amesema takriban nchi 40 Duniani zimeonesha nia ya kujiunga na #BRICS huku nchi 23 kati ya hizo zikiwa tayari zimetuma maombi kwenye kundi hilo ambalo kwasasa wanachama wake ni Brazil, Urusi,India,China na Afrika Kusini.
Mkutano wa BRICS umefanyika leo Agosti 24,2023 Johannesburg, Afrika kusini na umehudhuriwa na viongozi zaidi ya 50 kutoka Mataifa Yasiyo wanachama wa BRICS, akiwemo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.