TANZANIA YAKIRI BEI YA VANILLA KUSHUKA

0:00

Dar es salaam

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Hussein Bashe amesema sio kweli kwamba zao la Vanilla linauzwa kwa kilo Tsh .mil 1.5 ambapo amesema taarifa hizo ni za uongo huku akiwataka Waandishi wa habari kuisaidia Serikali kufikisha taarifa sahihi kwa wakulima kuhusu bei za mazao na taarifa nyingine za kilimo.

Bashe amesema hayo leo Ikulu Dar es salaam wakati akiongea na Viongozi pamoja na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF -AFRICA FOOD SYSTEMS SUMMIT 2023) ,unaotarajiwa kufanyika Septemba 05-08,2023 jijini Dar es salaam.

Kauli ya Bashe imekuja wakati akijibu swali lililotaka kujua bei halisi ya Vanilla,ambapo imekuwa ikitajwa bei ya kilo ni sh mil 1.5. Bashe anasema

“Nitaanza na swali la Mwandishi aliyeuliza je Vanilla inauzwa Mil 1.5 ni uongo,nimesikia iliandikwa na gazeti la Mwananchi ni vizuri kutokuchukua taarifa ambazo hazina ukweli ,kwakuwa nyinyi ni wanahabari ni vizuri vyombo vya habari mkalipia ada kidogo kujiunga kwenye International Commodity Platforms prices ambazo zinawasaidia kuona bei halisi za bidhaa Duniani kote lakini zipo Platforms kama Business Insiders ukiingia unaweza kuona bei halisi ya bidhaa fulani Duniani kwa wakati fulani”.

“Tanzania tunazalisha Vanilla kwa kiwango kidogo,Mikoa kama ya Kagera na Kilimanjaro Vanilla ni zao ambalo lina soko ,pareto sisi Tanzania ni wazalishaji wa pili Duniani lakini tunazalisha Tani Elfu 2 hadi 3 anayeongoza Duniani anazalisha Tani 8”

“Kwahiyo Vanilla zipo nchi ambazo zishapiga hatua sana Duniani zinazofanya vizuri kwenye zao hili ,Vanilla ilipanda bei miaka miwili mitatu baada ya Nchi ya Madagascar kukumbwa na vimbunga kwasababu wao ni wazalishaji waKubwa na sisi ikasaidia wakulima wetu kupata bei nzuri ,kwahiyo bei ya Tsh mil 1.5 haipo Duniani, bei ya laki 5 haipo Duniani “.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  SUALA LA RAIS SAMIA KUTOA SADAKA YA 5000 LIKO HIVI

Related Posts 📫

CBN has given PoS operators two months...
PROLIFIC NEWS CBN gives 1.9 million PoS Operators in Nigeria...
Read more
SAMIA ATOA NENO KUJIUZULU DANIEL CHONGOLO
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye Jamhuri yetu tukufu...
Read more
HOW TO KNOW THAT A GUY IS...
LOVE TIPS ❤ In this article, what I intend to...
Read more
Chelsea Interest in Philip Jorgensen has Developed...
It is just 10 days ago that we first heard...
Read more
Kenya Railways Unveils Luxurious SGR Executive Coaches...
The Kenya Railways has introduced new SGR (Standard Gauge Railway)...
Read more

Leave a Reply