Makala
Kwa mujibu wa utafiti wa Taasisi ya American Lung Association (ALA),vijana wenye kati ya miaka 18 hadi 24 Duniani wanazidi kuingia katika Matumizi ya “shisha” licha ya kilevi hicho kuwa na madhara ya kiafya.
Tafiti za ALA za mwaka 2020 zinaonesha 52.1% ya watumiaji wa shisha Duniani wanapatikana Afrika na Mashariki ya kati ambapo watumiaji wenye kati ya miaka 15 hadi 23 waliovuta shisha walikiri kilevi hicho kimewasukuma pia kuvuta Sigara.
Ikumbukwe, sigara ya Kawaida inahitaji kuvuta pumzi ndani kati ya mara 8 hadi 10 kwa sigara moja,wakati uvutaji shisha umetajwa kuhusisha uvutaji pumzi kati ya mara 100 hadi 200 kwa saa moja,kitendo kinachoingiza sumu ya Nicotine mara 1.7 ya wanaovuta sigara.
Mbali na kusababisha aina zaidi ya 7 za saratani ,shisha imetajwa kuwa sababu kuu ya saratani ya mapafu kutokana na Mtumiaji kuvuta kiasi kinachofikia Mikrogramu 90,000 za hewa yenye sumu kwa muda mfupi.
DONDOO
—
#Shisha inasababisha -matatizo ya Moyo
— Kuchakaa kwa ngozi
—- Kupoteza nguvu za kujamiiana
—– kuharibu fizi