Michezo.
Baada ya mkanganyiko uliotokea baina ya timu ya Yanga na beki wao Gift Fredy kuhusu kama ni kweli aliitwa timu ya Taifa ya Uganda au la sasa imebainika.
“Inawezekana Yanga walikuwa washaandaa bango ambalo ni uhakika kuitwa lakini baadae sasa ni kuyarusha tu bila kukagua sidhani kama mchezaji kadanganya! Taarifa inakuja kwa shirikisho, klabu halafu mchezaji”
“Au labda mchezaji alipewa za ndani akaomba ruhusa aondoke”
Huu ulikuwa mtazamo wa mchambuzi Alex Luambano wa Clouds Fm.
Lakini hiki ndicho kimemtokea mchezaji wa Yanga Gift Fredy anathibitisha David Kampista.
“Mlinzi wa Yanga Gift Fredy alijumuishwa katika kikosi cha The cranes akapata majeraha na kumfanya kocha Sredovic Milutin Micho kumuondoa ,barua ya kujumuishwa kwake ilitumwa kwa klabu kupitia kwa mamlaka husika ndio sababu klabu ilitoa taarifa ya kwamba ameitwa”.