Makala Fupi
Mapenzi yananoga wivu unapokuwa ndani yake. Ukitathimini kwa harakaharaka ,unaweza kusema kama hakuna wivu ,hakuna mapenzi. Inapotokea mpenzi wako, hata ufanye nini hakuonei wivu,bila Shaka hata wewe utahisi kuna tatizo.
Unatamani kale “kawivu” kidogo ili ujisikie unapendwa. Maana,tafsiri nyingine ya mtu asiyekuwa na wivu,huwa ni ile ya “wewe fanya yako, na mimi nifanye yangu,tusiingiliane”.
Wivu unapozidi kipimo ,nalo huwa ni tatizo lingine.Tunakubaliana hakuna ambaye atafurahia pindi asikiapo mwenzake amemsaliti. Ndiyo maana wapendanao hutumia nguvu nyingi sana kuhakikisha tu mwenzake hamsaliti.
Wapo ambao wanadiriki hata kuwawekea ulinzi wenza wao ili kuhakikisha kwamba kila kitakachofanywa na mpenzi wake anakijua . Kila eneo atakapokuwa mpenzi wake kunakuwa na watu wanaofikisha habari kama zilivyo.
Kundi la wanaume au wanawake wa aina hiyo ndiyo wale wanaokosa ustahimilivu akiona mpenzi wake amesimama na mtu tu barabarani,hana imani. Anatamani kujua wanazungumza nini ? Mpenzi wake akichelewa kurudi nyumbani, anatilia Shaka.