Michezo
Nyota wa Zamani wa AS Roma aliyewahi kutakiwa sana na Chelsea, Radja Nainggolan;
“Kama ningekuwa ninafikiria kuhusu pesa basi ningekuwa na maisha ya soka tofauti na niliyonayo kwasasa. Lakini sikuwahi kujali kuhusu pesa.Baada ya kutoka Cagliari ningejiunga na Juventus lakini pia baada ya kutoka AS Roma ningeweza kujiunga na Chelsea “.
“Nilisema sitokuja kujiunga na Juventus sio kwasababu ninaichukia Juventus kama baadhi ya watu walivyoandika kwenye mitandao ,lakini tu kwasababu nilitamani zaidi kucheza dhidi yao kuliko kucheza ndani ya Juventus. Sababu kubwa ni kwamba napenda kushinda dhidi ya timu ngumu”.
“Kwa miaka ile, Juventus ilikuwa timu imara na mimi nilitamani tu kucheza dhidi yao. Hiyo ndiyo nilijiwekea kama changamoto yangu . Kujiunga na Juventus Kisha nicheze mechi tano halafu timu ibebe Ubingwa kwangu sikuwa naiona kama njia ya kujiita bingwa”
“Wakati Antonio Conte akiwa kocha wa Chelsea, walijaribu pia kunisajili ,na walishangaa kiasi cha pesa nilichokuwa ninalipwa As Roma na wakataka kuniongezea mshahara karibu Euro 750,000 lakini sikutaka kwenda Uingereza kwa kiasi hicho cha pesa,ndiyo maana usajili ulivunjika”.