USIFANYE MAKOSA HAYA UNAPOKUWA KWENYE MAHUSIANO

0:00

Makala Fupi

Kilio cha wengi walio kwenye mahusiano ni kuhisi wanasalitiwa na wapenzi wao waliotokea kuwaamini haswa.Wapo ambao si tu kwamba wanahisi bali wanawakamata kila uchao wapenzi wao licha ya imani waliojenga kuwa wamepata wenza wa maisha.

Kiukweli kasi ya wapenzi kusalitiana imekuwa ikishika kasi kila siku kiasi cha baadhi kuhisi bila kusaliti hawajioni miamba na hii sio kwa wanaume hata wanawake. Yaani ,wanapata mahaba yote kutoka kwa wenza wao lakini bado tu mchepuko unaendelea. Unakuta mwanaume ana mke mzuri anayejua mapenzi na kila kitu lakini bado mwanaume huyo haridhiki na anachepuka.

Pia wapo wanawake ambao wamebahatika kuwapata wanaume “mabishoo” wanaojua mapenzi na kujali pia lakini bado tamaa za usaliti wanakuwa nazo . Ukiuliza kipi kigeni wanachofuata huko nje, huwezi kupata jibu la maana.

Nilishawahi kufanya uchunguzi huko nyuma kwa kuzungumza na baadhi ya wapenzi kuhusu hili suala la kusalitiwa.Wengi walikiri kujua kwamba kuna uwezekano mkubwa wapenzi wao wanawasaliti lakini wenyewe wanadai ni mambo ambayo wakiyafatilia sana wanaweza kujikuta wanaachana wakati huenda bado wanapendana.

HILO NDILO LINALOFANYA NIWE MPOLE ILA NAJUA HAKOSI MCHEPUKO NA NIKIMFUATILIA NAJUA WAZI KUWA NITAMFUMA ,TUTAGOMBANA NA HATA KUFIKIA HATUA YA KUACHANA ,SASA YA NINI HAYO?

“MAANA NINACHOJUA NI KWAMBA ,UKIMFATILIA SANA MPENZI WAKO UNATAFUTA SABABU ILI MUACHANE ,SASA KAMA HAUKO TAYARI MUACHANE NI VYEMA UKAMUAMINI NA KAMA HUKO PEMBENI ANA MCHEPUKO,NI YEYE NA MUNGU WAKE “

Alisema Dada mmoja ambaye kwasasa yuko kwenye ndoa huu mwaka wa 10.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  SABABU ZINAZOCHANGIA BIASHARA ZA WENGI KUFA HARAKA

Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading