FELICIEN KABUGA AACHILIWA HURU

0:00

Habari Kuu.

Rwanda iliamua kwamba inashikilia uamuzi wa kusimamisha kesi ya Felicien Kabuga kwa muda usiojulikana na kwamba ataachiliwa kwa muda na kuweka masharti ya kile kitakachofanyika.

Mwezi Machi mwaka huu,Mahakama ya The Hague, nchi Uholanzi ilisitisha kesi yake na mwezi Juni ikaamua kuwa Kabuga mwenye umri wa miaka 88 kwa mujibu wa nyaraka za mahakama ,hawezi kuendelea na kesi yake na baadae kuamua kwamba ataachiliwa kwa muda.

Uamuzi huu,ulilaaniwa na Serikali ya Rwanda na Mashirika ya waathiriwa wa mauaji ya kimbali . Kabuga anatuhumiwa kwa uharifu ,ikiwa ni pamoja na kuhamasisha moja kwa moja umma kufanya mauaji ya kimbali kwa kutumia Televisheni ya RTLM ,ambayo alikuwa ni mwanzilishi wake.

Kabuga ambaye hakuweza kujibu mashtaka dhidi yake kwasababu hakusimama kizimbani ,mwanzoni mwa kesi yake aliyaita mashtaka hayo uongo. Upande wa mashtaka ,ukiongozwa na Blamet ulikata rufaa dhidi ya uamuzi huu na uliomba kuwe na ziara ya pamoja mahali ambapo kabuga anazuiliwa kukagua afya yake.

Uamuzi mpya wa Mahakama, umewekwa kwamba,kikao kilichoongozwa na jaji Iron Nibonomy kilikataa ombi hili la upande wa mashtaka . Mahakama iliamuru kwamba wakati wa kusimamishwa ,kwa kesi kwa muda usiojulikana.

Kabuga ataendelea kuzuiliwa katika gereza la Umoja wa Mataifa, akisubiri uamuzi wa kuachiliwa kwake kwa muda. Mahakama ilisema kuwa ,afya yake itaendelea kufatiliwa gerezani na ripoti nyingine ya hali ya Kabuga inatarajiwa baada ya siku 180 kuanzia ile ya mwisho ya mwezi wa 8 na mashauriano zaidi kuhusu suala lake yataendelea kila baada ya siku 120 hadi atakapoachiliwa .

Mahakama iliamuru,upande wa mshitakiwa usaidiwe kuwasiliana na mamlaka ya chombo kilichohidhinishwa kuhusu nchi ambapo Kabuga anataka kuishi baada ya kuachiliwa kwake.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  ANTHONY MAVUNDE AFUTA LESENI ZA WACHIMBAJI MADINI

Related Posts 📫

Video ya Ayra Starr yashangaza mitandaoni
Read more
PAPA ATOA MSIMAMO WA KANISA KUHUSU MAPENZI...
HABARI KUU. Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani, Papa Francis, amesema...
Read more
Cardi B reportedly shared what she claims...
Cardi B has once again stirred the pot in her...
Read more
'Triple Crown' winner Pogacar on another level...
Slovenia's Tadej Pogacar is "a gear ahead" of the rest...
Read more
Sababu Kifo cha Yusuf Manji
Mfanyabiashara ambaye pia aliwahi kuwa Mfadhili na Mwenyekiti wa Klabu...
Read more

Leave a Reply