Juventus imesema kupita taarifa kwamba
Michezo
” klabu ya Juventus inatangaza kuwa leo 11 Septemba 2023 ,mchezaji wa mpira wa miguu Paul Liabile Pogba akipokea agizo la kusimamishwa kwa tahadhali kutoka Mahakama ya kitaifa ya kupambana na dawa zinazopigwa marufuku michezoni baada ya vipimo vilivyofanywa tarehe 20 Agosti 2023.
” Klabu inazingatia hatua zinazofuata za kiuratibu “
Ilisema taarifa ya Juventus.
Testosterone hormonal ,ambayo uongeza uvumilivu wa wanariadha . Pogba ana siku 3 za kufanya uchambuzi wa kupinga matokeo hayo .
Juventus ilimsajili tena Pogba kwa mkataba wa miaka 4 ,julai 2022 baada ya mchezaji huyo kumaliza mkataba wake na Manchester United na kuondoka kama mchezaji huru . Hata hivyo kurejea kwa Pogba huko Turin kumekubwa na matatizo ya mara kwa mara ya majeraha ambayo pia yalimfanya kukosa fainali ya kombe la Dunia, mwaka jana nchini Qatar.
Pogba amecheza jumla ya dakika 51 kama mchezaji wa akiba msimu huu katika mechi na Bologna na Empoli. Msimu uliopita alicheza dakika 108 katika mechi 6 za SERIE A .
Paul pogba anasema alifikiria kustaafu soka kwa madai ya udanganyifu na vitisho kutoka kwa genge lililopangwa ,akiwemo kaka yake Mattias.
Kiungo huyo wa kati wa Juventus mwenye miaka 30 aliwasilisha malalamishi kwa waendesha mashtaka wa Turin ,mnamo julai 2022 akidai kuwa analengwa na njama ya ulaghai ya pauni milioni 11.1 .