IFAHAMU SIMU MPYA YA IPHONE 15 ILIOZINDULIWA banner

0:00

Habari Kuu.

Kampuni ya Apple ,hapo jana Septemba 12,2023 ilizindua toleo jipya la simu zake za iPhone 15 Pro na iPhone 15 Pro max ambazo zimeboreshwa vitu mbalimbali na kuzifanya ziwe tofauti na simu nyingine za iPhone.

Jambo la kwanza ambalo lipo tofauti, simu hizi zimetengenezwa kwa madini ya Titanium yanayotumika kutengenezea ndege, na kuzifanya ziwe na uzito mwepesi ukilinganisha na iPhone nyingine lakini pia zikiwa na uimara wa hali ya juu.

Pia zimewekewa “Action Button “,kitufe kilichopo pembeni ya simu ambapo Mtumiaji anaweza kubadilisha anavyotaka na kufanya iwe rahisi kuitumia simu yake kwa kadri anavyotaka.

Kwenye suala la Camera,kama kawaida iPhone hawana jambo dogo au masiala ,iPhone 15 zimekuja na kamera ambazo zina lenzi yenye ubora mara saba zaidi ya zile zilizopo sokoni, kamera kubwa iliwa na 48 MP.

Kwa upande wa charger ,tofauti na iPhone nyingine zote ,iPhone 15 imekuja na chaja ya USB-C Connector wengi wanaita Charger Type C . Kizuri ni kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ,watumiaji wa simu za Android zinazotumia charger Type C,watakuwa na uwezo wa kubadilishana na watumiaji wa iPhone 15.

Mambo baadhi ya simu ya iPhone 15 ambayo itaingia sokoni rasmi Septemba 22,2023.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Dalili za mimba au ujauzito wa watoto...
Mimba ya mapacha ni hali ambapo mwanamke ana mimba inayobeba...
Read more
Super Schick nets four as Leverkusen thrash...
Bayer Leverkusen's Patrik Schick scored four times and Florian Wirtz...
Read more
MAGAZETI YA LEO 30 MEI 2024
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo kwenye...
Read more
Atalanta's Gasperini rues "cursed" Champions League draw...
Atalanta coach Gian Piero Gasperini was left frustrated after his...
Read more
WUMI TORIOLA EXPRESSES OVERWHELMING JOY AFTER PURCHASING...
CELEBRITIES
See also  WATU 50 WAJERUHIWA KWENYE NDEGE NEW ZEALAND
Actress Wumi Toriola expresses overwhelming joy after purchasing a...
Read more

Leave a Reply