Michezo
Video ya wimbo “Enjoy ” wa mwanamziki Juma Jux aliyomshirikisha Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinum imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kwasababu ya masuala ya haki miliki.
Akizungumza na kituo cha Habari cha Mpenja TV, Mwanamziki kutokea nchini Congo ,Sapologuano Odenumz ambaye ndiye alyeondoa “audio” ya wimbo huo mwezi mmoja uliopita amesema sababu za kuondoa video hiyo ni baada ya Msanii Jux kuvunja makubaliano waliyowekeana.
“Tulimalizana kimaongezi na vitu vingine ambavyo tumeongea nao tukamalizana nao siwezi nikaweka wazi kila kitu,lakini kuna baadhi ya vitu vingine ambavyo hawakutimiza ndio nimeamua kuishusha tena” amesema
Ameongeza
“Sisi hatuna ubaya nao ,mbele ya kufanya kitu chochote huwaga tunawajulisha kwanza,wanapokataa kutujibu tunaona kama hawa watu wanatugeuka na sisi tunafanya ya kwetu”.