HIZI NDIZO SABABU ZA IRAN KUMPA RONALDO SIMU

0:00

Michezo

Iran inataka kumpa laini ya simu ,Cristiano Ronaldo na wachezaji wengine wa soka wa kigeni ili kuwawezesha kutumia mtandao bila vikwazo watakapokuwa Tehran,huduma ambayo raia wa kawaida wa Iran hawawezi kufanya jambo linaloelezwa kuwakasirisha baadhi ya Wairan.

Reza Darvish ,Rais wa Persepolis FC, klabu ya kandanda ambayo itamenyana na Al Nassr ya Ronaldo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Asia.

Kiongozi huyo,kupitia kituo cha runinga cha taifa siku ya jana amenukuliwa akisema

Baadhi ya watu wanaotaka kuharibu sifa yetu wanawaambia wanasoka wasije Iran kwasababu hawataweza kufikia mtandao ambao haujachujwa”

Nimezungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Iran cell, na nikamwambia tunataka kuwapa wachezaji na wafanyakazi laini za IranCell zenye Internet isiyo nankikomo ili wazitumie kuanzia wanapoingia Iran hadi wakati wa kuondoka”

amesema.

Mtandao nchini Iran umewekewa vikwazo vikali,makumi kwa maelfu ya tovuti na majukwaa yote makuu ya kimataifa ya mawasiliano na mitandao ya kijamii yamezuiliwa.

Vizuizi viliongezwa kwa kiasi kikubwa baada ya katikati ya Septemba 2022 ilipoibuka ghadhabu ya watu kufuatia kifo cha Mahsa Amin aliyefia mikononi mwa polisi na kusababisha maandamano nchini kote ambayo yalidumu kwa miezi kadhaa.

Aidha, mamlaka nchini humo zinadai kuwa majukwaa ya kigeni,yalikuwa yanatumiwa kuhatarisha usalama wa Taifa, kwa kilichoelezwa kuunga mkono “machafuko” ndani ya mipaka ya Iran.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo...
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi Juni 01, 2024 na...
Read more
HOW TO KNOW IF THE LOVE IS...
When someone loves you, you know and you will feel...
Read more
TYPES OF MEN THAT MOST WOMEN PRAY...
LOVE ❤
See also  HOW TO KEEP PRIVACY IN A MARRIAGE
Ladies are always cautious in their interactions with...
Read more
South African champions Mamelodi Sundowns name Portuguese...
South African champions Mamelodi Sundowns, who will compete in next...
Read more
"I WAS BORN FOR PEOPLE TO LOOK...
OUR STAR 🌟 Popular reality star, Doyin brags about her...
Read more

Leave a Reply