Michezo
Kampuni ya Uwekezaji kutoka Marekani imefikia makubaliano ya kununua asilimia 94.1 ya hisa za klabu ya Everton kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri.
Kukamilika kwa dili hilo kunategemea idhini maalum kutoka kwa shirikisho la soka England (FA) ,hivyo utimilifu wake utaifanya Everton kuwa sehemu ya klabu zinamilikiwa na taasisi ya 777 ,ambayo pia inamiliki klabu kama Sevilla,Genoa,Hertha Berlin pamoja na Standard Liege ya Ubelgiji.
Licha ya aliyekuwa mmiliki wa klabu hiyo, Farhad Moshiri kuwekeza zaidi ya pauni milioni 750 tangu 2016,baadhi ya mashabiki wa Everton wamekuwa wakiupinga vikali utawala wa Moshiri ,kwa kufanya maandamano yaliyoshinikiza kung’atuka kwake.
Everton imedhamiria kupambana na kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja baada ya kuanza kusuasua huku kikosi cha Sean Dyche kikishika nafasi ya 18 kikiwa kimevuna alama moja pekee katika michezo minne ya Ligi ya EPL mpaka sasa.