Nyota wetu
Imeripotiwa kuwa jezi ya mchezaji mpya wa klabu ya Getafe ,Mason Greenwood, imevunja rekodi ya mauzo kwenye historia ya klabu hiyo ,kwa kuwa jezi iliyouzwa zaidi ndani ya wiki moja tangu kuwasili kwake klabuni hapo.
Mason Greenwood alijiunga na Getafe kwa mkopo akitokea Manchester united, baada ya kuwa na sintofahamu juu ya mustakabali wake.
Licha ya tuhuma zilizomkabili Greenwood, mwenye umri wa miaka 21 ,mashabiki takribani 4000 wa klabu ya Getafe walijitokeza uwanjani kushuhudia utambulisho wake,huku mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza akitarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Osasuna siku ya jumapili.
Pia, Mason Greenwood alipata mapokezi ya kipekee kutoka kwa Rais wa klabu hiyo ambaye walishiriki naye chakula cha usiku pamoja.
United ilihakikisha kuwa kinda huyo anapata makazi bora pamoja na mkalimani ,huku wakiendelea kulipa sehemu kubwa ya mshahara wa mshambuliaji huyo ambaye bado mpaka sasa wanatathimini njia nzuri ya kumrudisha Old Trafford.