Michezo
USM Alger imetwaa taji la CAF Super Cup ikiwachapa vigogo wa soka la Afrika mara 11, AL Ahly ya Misri kwa bao 1-0 katika mechi iliochezwa Dimba la King Fahd nchini Saudia Arabia.
Fainali ya CAF Super Cup imewakutanisha mabingwa wa ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly na wa kombe la shirikisho USM Alger kwa msimu uliopita.
USM Alger ilitwaa taji hilo la kwanza katika historia yao katika uwanja wao wa nyumbani licha ya Kupoteza mchezo huo 1-0 dhidi ya Yanga kwa bao la ugenini baada ya awali kushinda ugenini 2-1 katika Uwanja w Mkapa jiji Dar es salaam.
USM Alger inakuwa klabu ya pili nchini Algeria kushinda kombe hilo baada ya Wifak Setif mwaka 2015.
Vigogo Al Ahly iliwatoa mabingwa watetezi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wydad Casablanca kwa ushindi wa mabao 3-2.