Michezo
Ligi ya Mabingwa Afrika imeendelea leo kwa wawakilishi wa Tanzania Simba na Yanga kucheza michezo yao katika mataifa ya Rwanda na Zambia.
Simba Sc imemaliza dakika 90 za mechi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya wenyeji wao Power Dynamos katika Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia 🇿🇲.
Mabao ya Simba yote yamefungwa na Clatous Chama(58’90’) huku magoli ya Power Dynamo yakiwa ya kujifunga ya Henock Inonga 28 na Ayoub Lakred 74 na mchezo ujao utasubiri dakika nyingine za marudiano katika Uwanja wa Mkapa Octoba 1 mwaka huu kuamua yupi aendelee na hatua ya makundi?
Aidha, Yanga imetakata ugenini kwa kuipa kichapo Al Merrikh ya Sudan mabao 2-0 katika Uwanja wa Pele ,ikitanguliza mguu mmoja makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Washambuliaji Kennedy Musonda dakika ya 60 na Clement Mzize dakika ya 80 akipokea pasi ya kisigino ya Aziz Ki.