Makala Fupi
African Super Cup imeanzishwa rasmi mwaka 1993 lakini kabla ya hapo mwaka 1982 wazo hili lilianzishwa na katika mashindano ya undugu yalifanyika ambapo JS Kabylie bingwa wa klabu bingwa 1981 alicheza na Union Douala mshindi wa kombe la washindi na JS Kabylie walishinda kwa penati 4-3.
Tangu mwaka 1993 kuanza kwa mashindano ya Super Cup ya Afrika Al Ahly ya Misri ndiyo inaongoza kushinda mara nyingi ikishinda kombe hili mara 8 katika mashindano 11 ilioshiriki ,Zamalek wameshinda mara 4 huku TP MAZEMBE wakishinda mara 3. Timu za Misri zimeshinda mara 12 na zile za Morocco zimeshinda mara 5.
Katika mara 7 tu tangu kuanzishwa CAF SUPER CUP timu za Champions League zimepoteza kwq timu za kombe la Shirikisho ,mwaka 1993 Africa Sports d’Abijan waliwafunga Wydad Casablanca, ES Sahel waliwafunga Raja 1997,Maghreb de Fes waliwafunga ES Tunis mwaka 2019 na 2020,RS Berkane wakaifunga Wydad mwaka 2022 na USM Alger wameifunga Al Ahly mwaka 2023.
Miaka miwili mfululizo yaani mwaka 2022 na 2023 timu za Shirikisho zinazitambia zile za Champions League.
Mwaka huu sio Mwaka wa kwanza kwa bingwa wa Shirikisho kumfunga bingwa wa Champions League kwenye CAF SUPER CUP, na wala hiyo haijawahi kuondoa ugumu wa Champions League kulinganisha na kombe la Shirikisho.
Mashindano ya Champions League ya Afrika ndiyo Mashindano bora na magumu ya vilabu Afrika kuliko yale ya kombe la Shirikisho, hili ni dhahiri kwa mambo mengi ikiwemo zawadi za washindi ,Aina ya timu zinazoshiriki.