Habari Kuu
Jeshi la polisi nchini Uganda limeongeza juhudi za kupambana na magaidi nchini humo kwa kuanzisha zoezi la ukaguzi wa majumba ya serikali na watu binafsi kuona Kamera za CCTV zinafanya kazi hili kusaidia kutambua magaidi kwa urahisi.
Kwa mujibu wa polisi,sehemu zingine zinazotakiwa kufanyiwa ukaguzi kuweka kamera za CCTV ni pamoja na sehemu za mikusanyiko ya watu kama vile hospitali,soko,shule,vituo vya usafiri wa umma (mabasi,daladala),nyumba za ibada ,vituo vya mafuta ,baa na sehemu zingine za starehe nk
Msemaji wa polisi ,mkoa maalum wa Choga ,Afande Jimmy Okoma amesema
“Tunafanya ukaguzi katika majengo yote ya serikali na binafsi kuangalia utumiaji wa kamera za CCTV ,kufuatia vitisho vya magaidi nchini. Inakumbukwa hivi karibuni kulikuwa na vitisho katika jiji la Kampala na vitongoji vyake ,pamoja na baadhi ya mikoa . Mkuu wa kitengo cha polisi cha CCTV ,kutoka makao makuu ya polisi ametuma wataalam kushirikiana na wa mikoani kufanya ukaguzi kwenye majengo ya serikali na watu binafsi”
Hatua hii ya polisi ,inafuatia hotuba ya Rais Muse Museveni hivi majuzi ya kuongeza usalama katika sehemu za mikusanyiko na kuwataka waumini wa dini kuwa makini kwa watu wanaoingia kwenye nyumba za ibada na nyumba za wageni kuwaomba vitambulisho vyao kama hawafahamiki eneo hilo ,kuwazuia kuingia kwenye makanisa na misikiti.
Kwa mantiki hiyo Okema amesema suala la usalama sio suala la jeshi la polisi pekee,ni sharti kushirikiana na raia wote ,kufichua waaharifu kwa urahisi anaeleza
“Yote kwa hayo kuwa na ushirikiano na wadau katika kamera zao na kuungana na kamera za polisi kusaidia kufanya uchunguzi kwa haraka.Hii ni kutokana na kuwa jeshi la polisi haliwezi kupambana na uhalifu bila usaidizi wa raia kama inavyosema katiba ya Uganda, kifungu 21 kinapatia uwezo polisi na kifungu cha 17 raia wote wa Uganda. Hivyo natoa wito kwa wadau wote kushirikiana nasi katika zoezi hili “
Uganda bado inapambana na vitisho vya makundi ya kigaidi hasa wanaokisiwa kuwa waasi wa ADF . Mwanzoni mwa mwezi huu,walimkamata mtu mmoja aliyetaka kuingia na kifurushi cha bomu katika kanisa la Miracle Center Cathedral Lubaga ,mjini Kampala.
Jeshi la polisi walifanikiwa kutegua mabomu mengine matano yaliyokuwa yamepangwa kulipuliwa sehemu mbalimbali ya jiji la Kampala na kuwakamata watuumiwa 7 kufikia sasa kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Rais Museveni akihutubia taifa kuhusu hali ya usalama nchini humo .