MASHABIKI WA AJAX WAFANYA VURUGU KISA MATOKEO banner

0:00

Michezo

Nchini Uholanzi hapo jumapili kwenye mchezo kati ya Ajax na mtani wake wa jadi Feyenoord hali ilichafuka baada ya mashabiki wa Ajax kuzua vurugu zilizosababisha mchezo huo kusimamishwa.

Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki waliokuwa kwenye dimba la Johan Cruyff Arena. Vurugu zilianza tu baada ya Ajax kufungwa goli la 3 na Feyenoord ,ambapo mashabiki waliwasha fataki uwanjani hapo,hali iliozusha sintofahamu na mwamuzi kulazimika kusimamisha mchezo huo.

Pia, Askari wa farasi nao walilazimika kuwashughulikia mashabiki waliokuwa nje ya uwanja wakileta vurugu, huku timu yao ya Ajax ikiwa nyuma kwa mabao 3 na huku ikitajwa uharibifu kufanyika kwenye dimba hilo.

Mpaka sasa, Ajax inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi kuu Uholanzi, jambo ambalo mashabiki hawakulizoea kwa timu yao na huku msimu uliopita walipoteza Ubingwa wao wa Eredivisie kwa mahasimu wao ,timu ya Feyenoord Fc.

Kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo ,menejimenti iliamua kumtimua Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Sven Mislintat ambaye alichukua nafasi hiyo mapema mwezi Mei mwaka huu.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

FEELINGS YOU SHOULD MAKE YOUR SPOUSE FEEL...
LOVE ❤ 11 FEELINGS YOU SHOULD MAKE YOUR SPOUSE FEEL1....
Read more
Actor Femi Adebayo's Jagun Jagun bags seven...
Celebrated actor Femi Adebayo beams with pride as his film...
Read more
"WHY I DIVORCED KANYE WEST " Kim...
OUR STAR 🌟 American reality star Kim Kardashian has revealed...
Read more
SERIKALI YA TANZANIA KUPANUA BANDARI YA DAR...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaangalia namna ya...
Read more
SABABU YA MKE WA BILIONEA MSUYA KUACHIWA...
HABARI KUU
See also  ANAYETEGEMEWA KUSHINDA UCHAGUZI WA SENEGAL LEO
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar...
Read more

Leave a Reply