MASTORI
Wakati kocha Thomas Tuchel anaajiriwa ndani ya matajiri wa Ufaransa, PSG mwaka 2018 alipata dada wa kazi za ndani mwenye asili ya Ufilipino.
Maajabu ya dada wa kazi huyu ni kuwa ,alikuwa hafanyi kazi kama Thomas Tuchel na mke wake walivyozoea yaani mfanyakazi kufanya kwa masaa. Dada huyu ,muda wote alifanya kazi hasa ikizingatiwa, mke wa Bwana Thomas alikuwa ndio amejifungua.
Siku moja, Thomas Tuchel na mkewe walimuita huyo dada na kuongea nae kuhusu nini ilikuwa ndoto yake kwenye maisha? Dada alijibu kwamba angetamani siku moja awajengee wazazi wake huko Ufilipino,nyumba nzuri ya kuishi ambayo na yeye atakaa mpaka uzee wake. Thomas Tuchel na mkewe walicheka sana,lakini ukweli ni kwamba dada alimaanisha kweli alikuwa na uhitaji.
Baadae, Mkufunzi Tuchel alitimuliwa PSG na baadae akajiunga na matajiri wa London Chelsea ambao aliwasaidia kuwapa Ubingwa wa Ulaya (UEFA). Pamoja na kuamia nchini Uingereza, Tuchel alimjengea dada huyo nyumba yenye hadhi kwao Ufilipino ambapo huyo dada anaishi na familia yake.
MASTORI