MASTORI
Mshambuliaji mpya wa Bavarians ,muingereza Harry Kane amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudhani alifunga “hat-trick” (magoli 3) kwenye ligi kuu ya nchini Ujerumani “Bundesliga “.
Kwa baadhi ya nchi ,ikiwemo na Tanzania na hata England, ukifunga magoli 3 bila kujali umefunga kwa kipindi kimoja au vipindi viwili au kwenye muda wa nyongeza hiyo huwa ni “hat-trick” kama umetia kimiani magoli matatu (3).
Kwenye ligi kuu nchini Ujerumani, mambo ni tofauti kwani ,”hat-trick ” inahesabika pale tu unapofunga mabao matatu na yanatakiwa yawe ya kipindi kimoja na Kwenye kipindi hicho wakati unafunga haitakiwi mchezaji wa timu yako kufunga goli.
Kwahiyo, mpaka sasa bado Harry Kane hajafunga “hat-trick ” kwa mujibu wa kanuni za mpira wa Ujerumani “Bundesliga “.
MASTORI