Michezo
Nyota wa timu ya Al-Hilal ya nchini Saudia Arabia, Neymar Junior amesema hana furaha kufanya kazi na Mkufunzi Jorge Jesus. Hivi karibuni kumekuwepo na mvutano wa chinichini kati ya wawili ao .
Neymar Junior ambaye kwasasa hajafunga hata goli kwenye ligi hiyo anashinikiza kocha wake huyo aondoke ambaye kwa siku za hivi karibuni alimtaja Neymar kuwa “ana tabia mbaya”.
Pamoja, na kuwa Kwenye mgogoro huo wa chini kwa chini Al-Hilal imefanya vizuri ikiwa na ushindi Kwenye michezo 5 kati ya 7 ya ligi hiyo ,huku ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Al-ittihad inayoongoza kwa tofauti ya alama moja.
Neymar atalazimika kutumia ushawahi nje ya uwanja hasa kwa viongozi, iwapo hatopendelea kufanya kazi na kocha Jorge Jesus ambaye ni kocha mkuu wa Al-Hilal.
Mbrazil huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo akitokea PSG kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 75 ,mwezi mmoja uliopita. Amecheza jumla ya mechi tatu bila kutupia goli hata moja,kitendo kinachomnyima usingizi huku akikosoa vikali mbinu za kocha.