NYOTA WETU.
Toka kwenye uumbaji imeonekana Mwanamke ana nguvu sana kwenye mahusiano yoyote. MUNGU alipomuumba Adam na Eva (Hawa) ,agizo la kwanza alilompa Adam ni kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Katika hali isiyo ya kawaida kwa ushawishi wa Mwanamke (Eva) ,Adam alimkosea MUNGU na kula matunda. Hali ilienda mpaka kwenye kizazi za Samson na Delila, Yosefu na Cleopatra na wengine wengi mpaka kwa Bill Gates na mkewe Melinda Gates ,ambapo Mwanamke amekuwa ni kinara wa mambo.
Nyota wa zamani wa Marseille, Arsenal na Galatasaray mwenye asili ya Ivory Coast Emmanuel Ebouè ,mnamo mwaka 2017 alitangaza kufilisika ni baada ya mkewe Aurelia kufanikiwa kuchukua Mali zote ikiwemo na watoto 3 yaani Matts, Clara na Maeva kutokana na kesi ya kutalakiana. kwasasa Ebouè amefikia hatua ya kutangatanga kwa kukosa makazi maalum ya kuishi na huku mtalaka wake akiendelea kula maisha.
Mwaka 2023 ,gumzo lilikuwa kwa kijana wa miaka 25 na mchezaji wa klabu ya PSG Achraf Hakimi ambaye alifanikiwa kumshinda Mwanamke alietaka kuchukua mali zao kwa kile ambacho mwanamama huyo Hiba Abouk alitaka talaka. Kwenye kesi,ilikuja kuonekana Hakimi hana chochote cha kugawana na Mwanamke huyo kwani mali ni za mama yake Hakimi. Jambo hili limekuwa likiwatesa nyota wa Afrika wanaofanya kazi Ulaya na Marekani, ambapo wanawake makahaba ujiingiza Kwenye mahusiano na nyota hao na baadae uomba talaka, hili tu wagawane mali.
Huko ni kwa wenzetu,lakini na hapa kwenye nchi yetu tuna nyota ambao nao kwa kujua waliingia kwenye mahusiano lakini baada ya kushindwa kuendelea vizuri kwenye mahusiano, sababu huwa inatajwa ni matumizi ya fedha. Diamond Platinum ni miongoni mwa nyota nchini ambaye amekuwa na vimwana kama Zari The Bosslady, Tanasha Dona,Fontana nk Hawa ni baadhi ya vimwana wanaotoka kwenye familia za hela tofauti na Zuchu au Hamisa.
Wengi wa wasiolewa,kuna ugumu mno ukiwa na kipato kidogo kuishi na Zari au Tanasha Donna. Hawa ni wanawake, ukiwa nae lazima utabadilisha hali yako ya kuishi kwani malazi na maisha yako lazima yawe tofauti na ambavyo utaishi na Zuchu. Wengi watasema Diamond Platinum kuishi na Zuchu ni kujishusha kwani sio Mwanamke wa hadhi yake lakini ukweli ni kwamba ni mara 100 kuishi na Zuchu kuliko kuishi na Zari.
Hata Alikiba na mkewe wamekuwa kwenye msuguano huku ikitajwa Alikiba anamsaliti lakini mambo ndio yale yale,kuishi na wanawake wa nje inagharimu mno kuliko pale unapokuwa na mzawa.
Wengi wa wanawake hasa wanaojielewa ,Matumizi yao ni makubwa kwasababu wao hawaji kuolewa bali kutumia hela ambazo kama unazo basi zitaanza kupungua hasa kwa wanaozitafuta bado. Wageni hawa ,wanaolewa kwa muda na baadae wanaomba talaka ili mgawane mlicho nacho. Kwa hili sasa ,huenda kweli hata Diamond Platinum akuwahi kusema lakini ukweli wa mambo huko hivi.