Makala Fupi
Leo mtandao wa Google umetimiza miaka 25 tangu ulipoanzishwa mwaka 1998 na wanafunzi Larry Page na Sergey Brin wa chuo cha Stanford ,jimbo la California wakiwa ni wanafunzi wa elimu ya juu ya sayansi ya computer.
Wanafunzi hawa walikuwa na malengo ya kuunda mtandao ambao ungeweza kukusanya wavuti ambazo huzalisha makusanyo ya Data. Mtandao wao kwa mara ya kwanza uliitwa Backrub kabla ya kuamua kubadili jina lake na kuuita Google.
Kwasasa Google inamiliki mtandao wa Gmail,YouTube na utafutaji yaani Search engine. Mtandao huu ambao unatumiwa na mabilioni ya watu Ulimwenguni, umekuwa msaada wa mapinduzi kwa ambao wangependelea kupata taarifa mbalimbali.
Wengi wa watumiaji, wamekuwa wakiamini taarifa za Google ambayo pamoja na mambo mengine imejitahidi kuchuja baadhi ya maudhui ambao sio au hayaendani na maadili na pia Google hufanya biashara na makampuni makubwa Duniani yakiwemo ya Usafirishaji,Vinywaji,burudani nk huku pia ikitoa malipo kwa watumiaji wa mtandao wake wenye haki ya kupata malipo kwa njia ya matangazo.
Vijana hao wawili walioanzisha mtandao huu wakiwa bwenini,wanatajwa ni mabilionea ulimwenguni kwa miaka mingi mtawalia na huku mtandao huo kwa sasa ukiwa na ukwasi wa $1.675 trioni.