Habari Kuu
Nchi za Kenya 🇰🇪, Tanzania 🇹🇿 na Uganda 🇺🇬 zimepitishwa kuandaa michuano mikubwa ya soka barani Afrika yaani kombe la Mataifa ya Afrika(AFRICON) taarifa ya CAF imetaja mapema hivi leo.
Nchi hizi za Afrika Mashariki zimepata zabuni hii baada ya kuwaangusha washindani wao Misri 🇪🇬 , Senegal 🇸🇳, Botswana 🇧🇼 na Algeria 🇩🇿 ambaye alijitoa siku mbili kabla ya kutangazwa mshindi hivi leo.
Morocco ambaye aliiandaa michuano ya AFRICON kwa mara ya mwisho mwaka 1998 alipewa uandaaji huo mwaka 2015,ambapo alishindwa kuandaa michuano hiyo kwa kisingizio cha ugonjwa wa Ebola nchini mwake,2025 ndio atakuwa muandaaji wa AFRICON kabla ya kuwaachia Tanzania, Kenya na Uganda.
Kwa historia ya mpira Afrika, itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuandaa michuano ya AFRICON ilionzishwa mwaka 1957 ambapo toka mwaka 1968 imekuwa ikichezwa baada ya miaka 2 na mapema 2013 kulitokea mabadiliko yaliyopelekea kutoka kwenye mwaka unaogawanyika kwa 2 mpaka kwenye mwaka usiogawanyika kwa 2 mpaka sasa.