Michezo
Kwa mujibu wa jarida la Bloomberg, wamiliki wapya wa Chelsea wanapanga kukopa paundi 250 milioni kwa ajili ya kuingia sokoni kununua wachezaji wapya.
Pamoja na mpango mkakati huo wamiliki hao watakwaa kisiki kutokana na kipengele cha mkataba walichowekeana ,wakati Roman Abramovich akishinikizwa kuiuza klabu ya Chelsea. Kipengele hicho cha mkataba kinasema ,wamiliki wapya hawatakiwi kukopa kwa jina la Chelsea ndani ya kipindi cha miaka 10 ya umiliki.
Kipengele cha mkataba hicho kimepewa jina la Anti-Glazer ,kikichukuwa jina la wamiliki wa timu ya Manchester United na wamiliki wake Glazers Family ambapo, walikopa kiasi kikubwa cha pesa kwa jina la Manchester na kuitwisha klabu mzigo.
Kama hali itaendelea hivi ni kwamba, wamiliki hawa wapya watakopa kwa jina lao ambalo Kwasasa ni Blue Co hali ambayo haitaathiri na kuitwisha klabu mzigo mpya wa madeni.
Chelsea imekuwa chini ya umiliki wa Roman Abramovich toka mwaka 2003 huku ikitwaa makombe lukuki ya ligi ya EPL na Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwasasa ipo chini ya wamiliki wapya baada ya Roman kulazimishwa kuiuza baada ya Urusi kuivamia Ukraine, kwa kile kilichotajwa Roman Abramovich ni rafiki wa karibu wa Vladimir Putin.