Makala Fupi
Leo imekuwa siku ya kihistoria baada ya Mteule ,Mhadhama Protas Kadinali Rugambwa kutawazwa kuwa Kadinali mpya kutokea Tanzania. Huyu anakuwa Kadinali wa 3 baada ya Lauren Rugambwa, Polycap Pengo na sasa ni Protas Rugambwa mzaliwa wa Kagera Karagwe.
MAJUKUMU YA KADINALI
Kwa mujibu wa kanisa katoliki,Kiongozi mkuu ni Papa ambaye uchaguliwa na Makadinali kutokea Duniani kote. Utawala wa kanisa la Roma hauko tofauti na utawala wa kawaida wa serikali, ambapo Papa anasimama kama Rais huku Makadinali wakiwa kama ni mawaziri wake.
Majukumu makubwa ya Makadinali ni kuwa Kwenye baraza kuu la Makadinali (curia) ambalo uongozwa na Papa,kumchagua Papa kama amefariki au kuachia madaraka yake na pia kuchaguliwa iwapo Papa amefariki au kuachia ngazi. Kwenye Majukumu ya kila siku kuna Kadinali mwenye wajibu wa kuwasimamia Maaskofu wote wa Dunia nzima, kuna Kadinali anayehusika na Injili Dunia nzima,kuna Kadinali anahusika na miundombinu ya Dunia nzima nk.
Kadinali anaposimama au kuzungumza huwa ni kwa niaba ya Baba Mtakatifu ,kwahiyo Kadinali anasimamia majukumu yote ya Papa pasi na shaka. Kadinali pia ana heshima zote za kipapa na anaingia sehemu au nchi yoyote Duniani bila ya visa.