NYOTA WETU
Mkongwe wa soka David Beckham ametolea ufafanuzi uamuzi wake wa kuwa balozi wa kombe la Dunia nchini Qatar, ambalo lilikuwa dili nono lililokosolewa vikali.
Akizungumza na tovuti ya The Telegraph nyota huyo wa zamani wa England amesema;-
“Huwa nafanya utafiti kwa washirika ninao kwenda kufanya nao biashara, na nilitaka kuwa sehemu ya kombe la Dunia “.
“Napenda kuiona soka inakuwa ,ndio maana napenda kuona soka sehemu ambayo haijawahi kwenda kabla”
“Nilijuwa yatakuwepo maswali,nitakosolewa,hata hivyo siku zote nimekuwa nikiamini soka kitu chenye nguvu”.
“Nilikaa kule mwezi mzima,na hakuna mtu hata mmoja aliyenifuata na kusema,”ooh nimetendewa hivi ,ooh nimetengwa,sikukubaliwa kuingia hapa au pale.Hivyo, uamuzi wangu wa kufanya kazi na Qatar niliufurahia”.
Beckham ana mkataba wa miaka 10 kama balozi wa Qatar. Mkataba huo wa ubalozi unatajwa kumuingizia paundi milioni 125.