Michezo
Baada ya kuitikisa Ulaya kwa kusajili wachezaji nyota kwenye msimu huu ,sasa Ligi kuu ya Saudia Arabia inatarajia kuajiri waamuzi kutoka pia barani humo. Waamuzi kutoka England wanatazamwa kwa jicho sana.
Katika hatua ya kuendeleza ligi kuu ya Saudia Arabia, waamuzi kutoka nchi kama New Zealand, Paraguay 🇵🇾 na Argentina 🇦🇷 walitumika kwenye michezo maalum. Hata hivyo, Saudia Arabia pro League ,inalenga kutoa kandarasi za msimu mzima,zenye mshahara mnono kwa waamuzi kutoka barani Ulaya.
Kwa wastani,mwamuzi wa kiwango cha juu Ligi kuu England, hulipwa kati ya paundi 120,000 mpaka paundi 300,000 kwa mwaka,kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail.
Hivyo, Ligi kuu ya Saudia Arabia imelenga kutoa nyongeza kubwa ya mishahara na makato madogo ya kodi hili kuvutia waamuzi kwenye ligi hiyo maarufu kama Saudia Arabia pro League.
Mwezi April, Mwamuzi kutoka ligi kuu ya England, Michael Oliver, alilipwa takribani paundi 3,000 kuamua kwenye mchezo wa Al-Hilal na Al-Nassr ,ya Cristiano Ronaldo, ikitajwa kuwa zaidi ya kiasi anachoingiza kwenye mchezo mmoja kwenye ligi kuu ya England.
Hofu imetanda juu ya ligi hiyo pendwa Ulimwenguni kupoteza waamuzi bora ,huku vyombo mbalimbali vikiripoti kuwa ,uamuzi huo utapingwa vikali.