HABARI KUU.
Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani, Papa Francis, amesema atakuwa tayari kuona kanisa katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja lakini sio kwa makuhani wanawake, katika majibu yake ya hivi karibuni kwa Makadinali ambao walikuwa na maswali kuhusu msimamo wa Papa kwa jamii ya LGBTQ katika kanisa katoliki.
“Hatuwezi kuwahukumu ambao wanakanusha tu,kuwakataa na kuwatenga”. Na kuongeza kuwa ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na “hisani ya kichungaji”.
Hata hivyo,Kanisa katoliki bado linachukulia mapenzi ya jinsia moja “kuwa dhambi” na halitatambua ndoa za jinsi hiyo.
Jibu la Papa Francis kwenye kurasa nane (8) ,lilitolewa na Vatican siku ya jumatatu ,Octoba 2 linaonesha majibu yake kwa Makadinali watano wa kikatoliki waliostaafu ambao wameeleza wasiwasi wao kuhusu masuala kadhaa yenye utata yanatarajiwa kujadiliwa kwenye sinodi (Mkutano wa Maaskofu),ambao utaanza Octoba 4 mpaka 29.