MWENYE SEHEMU ZA SIRI MBILI AONDOLEWA UKE

0:00

HABARI KUU

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke imefanyia upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike (uke) kutoka kwenye korodani ya mgonjwa wa jinsia mbili mwenye mwonekano wa jinsia ya kiume ikiwa ni mara ya kwanza upasuaji huo kufanyika katika hospitali za rufaa zilizopo Tanzania.

Upasuaji huo umefanywa na jopo la Madaktari kutoka hospitali hiyo, na limeongozwa na daktari Bingwa wa upasuaji wa jumla na mfumo wa mkojo,Dkt Hussein Msuma pamoja na wasaidizi wake ,Dkt. Hamis Mbarouk ,Curtuis Mbalamula ,Mkati na Shani Maupa.

Taarifa ya hospitali hiyo imeeleza kuwa kufanyika kwa upasuaji huo ni moja ya mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya Tanzania kwa kuwa moja ya jitihada za serikali na Wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha hospitali zina uwezo wa kutoa matibabu ya kibingwa na Ubingwa bobezi.

Akizungumza baada ya upasuaji kufanyika na kufanya vipimo vya sampuli zilizotolewa katika upasuaji, Dkt Msuma amesema mgonjwa alifika hospitalini akiwa na mwonekano wa jinsia ya kiume lakini ana maumbile ya ndani ya aina mbili ,yaani maumbile ya kiume na kike ,hivyo kupelekea upasuaji huo.

“Alikuwa na mifumo ya uzazi ya jinsia mbili,ya kiume kwenye korodani ya kulia na ya kike kwenye korodani ya kushoto “

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

TIMU ZINAZOWANIA KUMNASA PRINCE DUBE Uongozi wa...
Read more
ERIC TEN HAG KUTIMULIWA MANCHESTER UNITED
Tangu mwaka 1990 miaka 34 sasa Klabu ya Manchester United...
Read more
World number one Jannik Sinner has withdrawn...
The Italian struggled with illness during his Wimbledon quarter-final loss...
Read more
SEX AND MARITAL PROBLEMS EDUCATION
Sex doesn't solve marital problems. You two can have great...
Read more
See also  Kwanini Donald Trump ana Nafasi ya Kushinda Urais wa Marekani?

Leave a Reply