Michezo
Nahodha wa klabu ya Chelsea, Reece James, amefungiwa mechi moja pamoja na pamoja na faini ya paundi 90k zaidi ya TZS 270 milioni, kwa kosa la matumizi ya lugha isiofaa michezoni kwa Afisa wa mechi baada ya mchezo wa Chelsea na Aston villa kuisha kwa Chelsea kukubali kichapo cha 1-0.
Mlinzi huyo wa pembeni alikiri makosa ,kwa kumtusi na kunena maneno machafu kwa Afisa wa mechi kwenye njia ya kuelekea vyumba vya kubadilisha nguo ,baada ya mchezo huo kutamatika.
Tukio hilo linalinganishwa na la Nahodha wa Liverpool, Virgil Van Dijk ,wakati alipomtusi mwamuzi, John Brooks, kufuatia kadi nyekundu dhidi ya Newcastle mwezi Agosti.
James,ambaye ni majeruhi ,hakuwa kwenye kikosi kilichoikabili Villa ,lakini aliripotiwa kwa mamlaka za soka England FA kufuatia tabia yake dhidi ya mwamuzi Jarred Garrett, ambaye alihusimamia mchezo huo kwenye dimba la Stamford Bridge, mnamo Septemba 24.
Marufuku hiyo ya James, ilitakiwa kutimia kwenye mechi dhidi ya Burnley siku ya jumamosi,hata hivyo tatizo lake la misuli ya paja linamaanisha kwamba hatohusika kwenye mchezo huo.
James, anaweza kurejea uwanjani Oktoba 21,pindi Chelsea itakapoikabili Arsenal, baada ya mechi za kimataifa.