MAKALA FUPI
Mtandao wa wahalifu umefichuliwa nchini Pakistan 🇵🇰 ambao wakati mwingine hukata figo za watu bila wao kufahamu.
Watu nane walikamatwa kwenye msako akiwepo na daktari. Waliweza kumiliki figo za watu bila kufuata sheria huku wakiwa na akiba zaidi ya figo kwaajili ya kuwapandikiza watu hasa matajiri.
Kulingana na mamlaka, baadhi ya wafadhili hawakukubaliana na oparesheni hiyo.
Mkuu wa Serikali katika jimbo la Punjab Pakistan, Mohsin Naqvi,alisema katika mkutano wa waandishi wa habari jumapili kwamba Dk.Fawad Mukhtar alifanya upasuaji wa kuondoa figo nyumbani kwake na mara nyingi bila idhini ya wagonjwa na wanaofadhili.
Kulingana na Naqvi, fundi wa magari kwa taaluma alimsaidia daktari kama msaidizi wake katika operesheni; pia alisaidia kwenye katika kuwakusanya wagonjwa wa hospitali kwaajili ya upasuaji.
Kwahiyo, walifanya angalau operesheni 328 ,kama ambapo watoaji angalau watatu walifariki.
Kulingana na wachunguzi, waliokamatwa waliuza figo kwa wageni kwa rupia milioni 10 (sawa na dola 120,000) na kwa wagonjwa wa Pakistan kwa rupia milioni 3.
Mohsin Naqvi alisema kuwa Dkt.Mukhtar alikamatwa mara tano hapo awali ,lakini kila mara aliachiliwa kwa usaidizi wa maafisa wa polisi mafisadi.
Genge hilo liliendesha shughuli zake hasa Lahore,Jiji lenye watu takribani milioni 13 ,Taxila,karibu na mji mkuu wa Islamabad, na pia katika sehemu ya Pakistan ya Kashmir.