URUSI YAFANYA MAJARIBIO YA NYUKLIA

0:00

HABARI KUU.

Urusi imefanya “Jaribio la mwisho lililofanikiwa” la kombora la Nyuklia , Vladimir Putin amedai.

Maoni ya Rais yamewadia baada ya msemaji wake kukataa maoni ya The New York Times kwamba majaribio ya silaha ,inayojulikana kama Burevestink ,yalikuwa yanakaribia.

Silaha iliofanyiwa majaribio, ilitangazwa kwa mara ya kwanza mnamo 2018,kna ilisifika kama silaha yenye kusafiri masafa marefu bila ukomo.

Lakini ni taarifa kidogo sana rasmi zinazojulikana kuhusu uwezo wake na kuna ripoti ya kwamba majaribio ya awali yalikwenda mrama.

Walakini, picha za setelaiti zilizosambazwa mwezi uliopita zilionyesha kuwa Urusi ilikuwa imejenga vifaa vipya hivi karibuni katika eneo la mbali la kisiwa cha Aktiki ambapo majaribio ya Nyuklia ya Soviet yalifanyika hapo awali.

Picha hizo zilionyesha kazi ya ujenzi huko Novaya Zemlya ,kisiwa kilicho Kaskazini mwa Bahari ya Barents.

“Sasa tumemaliza kazi za aina ya kisasa za silaha za kimkakati ambazo nimezizungumzia na nilitangaza miaka michache iliopita “,

Bwana Putin aliambia mkutano katika eneo la mapumziko la Bahari nyeusi huko Sochi mnamo Alhamisi ambao ulirushwa moja kwa moja kwenye runinga ya serikali.

Aliongeza,

“Jaribio la mwisho lililofanikiwa limefanyika Burevestink- kombora la kimataifa linalotumia nguvu za Nyuklia “.

Kombora hilo lililopewa jina la Skyfall na NATO ,linasemekana kuendeshwa na kinu cha Nyuklia,ambacho kinatakiwa kuwashwa baada ya viboreshaji vya roketi za mafuta kulirusha angani.

Lakini gazeti la The New York Times lilinukuu kundi la kampeini ya kuthibiti silaha ,Nuclear Threat initiatives, likisema kwamba majaribio 13 ya awali ya mfumo huo ya kati 2017 mpaka 2019 yote hayakufaulu.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Andy Murray has confirmed he will retire...
The 37-year-old is planning to play in the singles and...
Read more
Verstappen stuns in Sao Paulo with win...
SAO PAULO, - Red Bull's Max Verstappen had his fourth...
Read more
WHY YOUR SPOUSE REJECTS YOU
LOVE ❤
See also  MAMBO MAKUU 4 YA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA TENDO LA NDOA
12 BAD MOODS WHY YOUR SPOUSE REJECTS YOU...
Read more
HABITS OF BABY HUSBAND
Food rejection:. You are the owner of the food and...
Read more
A video featuring Wizkid, Mayorkun, and BNXN...
CELEBRITIES Amidst the ongoing feud between Davido, Wizkid, and BNXN,...
Read more

Leave a Reply