MAKALA
Govi ni sehemu ya juu ya uume inayofunika sehemu ya juu ya uume. Tofauti na sehemu ya ngozi inayobaki ,ambayo imeshikamana na uume ,govi limejitenga na,ikiwa hakuna shida,inapaswa kutolewa mpaka uume wote uonekane ,katika hali ya ulaini ya uume kusimama.
Sehemu ya ndani ya govi huwa sawa na sehemu ndani ya mdomo au ndani ya uke wa Mwanamke ,
“Kazi yake ni kufunika kiungo ,hutumika kama kifuniko”
Mtaalamu wa masuala ya mfumo wa mkojo Ana Maria Autran ,kutoka Shirikisho la Marekani, aliiambia BBC Mundo. Wataalamu wana amini inaweza kuwa na kazi maalum ya Kinga.
Hata hivyo, mwanaume anaweza kuishi bila govi. Lakini sehemu hiyo ya juu ya mwanaume ni sehemu nyeti sana. Wakati govi linapoondolewa kwa sababu za kiafya katika ujana,utoto,au utu uzima,sehemu ya juu ya uume, sehemu ya juu ambayo ilikuwa imelindwa hapo awali, hugusana moja kwa moja na nguo na hewa.
Kwa sababu hii,mgonjwa huwa anapata usumbufu hasa kwenye wiki ya kwanza kutokana na sehemu hii kugusa nguo. Anaweza,kwa upande wake, kuhisi maumivu makali wakati wa kusimama kwa uume.
Baada ya muda ,ngozi ya uume inakuwa ngumu na kupoteza hisia fulani.
Upasuaji kwa upande wake unafznyika kwa njia mbili: njia ya jadi na njia ya hospitali ambapo anayetolewa govi upewa dawa maalum ya usingizi ili kuondoa sehemu hiyo nyeti ya uume.