Michezo
Meneja wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amefiwa na mke wake Lady Cathy Ferguson ambaye ameaga Dunia akiwa na umri wa miaka 84 na kuacha watoto watatu ,wajukuu 12 na kitukuu 1.
Katika taarifa yake leo Oktoba 6,2023 Manchester United imesema,
“Kila mmoja ndani ya Manchester United anatuma salamu za rambirambi kwa Sir Alex Ferguson na familia yake kwa kuondokewa na Lady Cathy “
“Kama ishara ya heshima, wachezaji wetu watavaa kitambaa cheusi wakati wa mechi ya Jumamosi dhidi ya Brentford “
Imesema taarifa hiyo.
Bendera kwenye uwanja wa Old Trafford zimeshushwa nusu mlingoti huku timu za wanawake na wanaume za klabu hiyo zitakazocheza mwisho wa wiki hii zitavaa vitambaa vyeusi kama ishara ya kuomboleza msiba huo .
Sir Alex Ferguson aliiongoza Manchester United kwa miaka 26 na inatajwa Bodi ya Manchester United iliwahi kuwa na mgogoro na Sir Alex Ferguson mnamo mwaka 2001 ambapo Sir Alex alikuwa tayari kuachia ngazi kama kocha lakini kwa ushawishi wa mke wake aliamua kusalia Old Trafford mpaka mwaka 2013 alipotangaza kustaafu.