MAKALA
Katika baadhi ya maeneo ya Afrika, watu wanakabiliwa na ukosefu wa makazi kutokana na sababu kadhaa. Kuna nchi zinakumbwa na mapigano ya mara kwa mara ambapo silaha nzito hutumika,jambo hili huchangia pakubwa watu kukimbia kwa kuhofia usalama wa maisha yao.
Pia,kuna sababu za kiuchumi nazo zinachangia pakubwa kuishi Mitaani au makazi duni.
Ukosefu wa ajira pia unachangia pakubwa watu kukosa makazi maalumu ya kuishi hasa kwa maeneo ya mijini ambapo inatajwa gharama za maisha ziko juu.
Makazi duni na mazingira magumu katika baadhi ya maeneo, huchangia pia kuongezeka kwa watu wasio na makazi .Hii inaweza kuchangia kuongezeka kwa magonjwa, uharifu ,na hali ngumu kwa watu hao.
Kwa Afrika nchi hizi ni pamoja na:-
1. NIGERIA 🇳🇬 Mi24.4
2. MISRI 🇪🇬 Mil 12
3. DRC CONGO 🇨🇩 Mil 5.3
4. SOMALIA 🇸🇴 Mil 2.9
5. SUDAN 🇸🇩 Mil 2.73
6. ETHIOPIA 🇪🇹 Mil 2.7
7. SUDAN YA KUSINI 🇸🇸 mil 1.54
8. CAMEROON 🇨🇲 Mil 1.03
9. MOZAMBIQUE 🇲🇿 769,000
10. BURKINA FASO 🇧🇫 700,000