MASTORI
Mwaka 2020 wakati Loic Remmy alipomzungumzia Eden Hazard;
“Nilimjua Eden Hazard hata kabla sijajiunga na Chelsea. Nilikuwa nacheza dhidi yake wakati huo nilikuwa mchezaji wa Marseille na Nice yeye akiwa mchezaji wa Lille.

“Nilipofika Chelsea na kushiriki mazoezi kwa mara ya kwanza, Eden alifika akiwa hajafunga kamba za viatu na alinikaribisha. Nikamuuliza,utafanya mazoezi ukiwa hivyo?Alinijibu ndio,hakuna tatizo.
“Binafsi yangu nilikuwa najua nikifika Chelsea nitakuta timu inafanya mazoezi kwa nguvu sana kwasababu ni klabu kubwa na nikajiwekea malengo kwamba nitapambana kwa nguvu zote. Lakini nilipomwangalia Hazard nilishangaa.
“Ikafika siku ya mechi ambayo ilikuwa kwangu mechi ya kwanza, ilikuwa dhidi ya Swansea City (Septemba 2014).Nilianza nikiwa benchi na Diego Costa alifunga magoli matatu,Jose Mournho akanipa nafasi ,niliingia na kufunga goli langu la kwanza lakini hiyo ilikuwa baada Eden kucheza kwa ustadi mkubwa Kisha kumpa pasi Oscar ambaye ndiye alinipasia”
“Nilipoenda kwenye chumba cha kubadilisha nguo nilifurahi sana,Kisha Eden alinifuata na kuniambia ,”si umeona? Mimi ndiye boss” Na kweli alikuwa boss kwasababu alifanya mambo kuwa marahisi. Ni mchezaji mwenye akili sana.”.