RAIS SAMIA AINGIA KWENYE ORODHA YA GOOGLE

0:00

NYOTA WETU

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mtu wa pili kwa habari zake kutafutwa sana nchini India kuliko kitu kingine chochote katika mtandao wa Google nchini India ambao ndio mtandao maarufu Duniani kote.

Nafasi ya kwanza ilishikwa na nyota wa kriketi kutoka Pakistan, Babar Azam,ambaye jana alicheza vibaya kiasi cha kutolewa kwenye mechi dhidi ya Pakistan, ikumbukwe kuwa mchezo wa kriketi ndio mchezo pendwa India kuliko mchezo wowote ule.

Licha ya siku ya jana Rais wa India 🇮🇳 na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Amartya Sen alifariki Dunia lakini alizidiwa kwa kufatiliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwingine ni nyota wa kambumbu wa zamani wa vilabu vya Lille ,Chelsea na Real Madrid na timu ya Taifa Ubelgiji Eden Hazard alichukua nafasi ya nne kwa kufuatiliwa zaidi mitandaoni.

India ni taifa lenye idadi ya watu bilioni moja na milioni mia tatu sawa na takribani mara 21 ya watanzania wote na huku ikitajwa kama nchi kinara kwa matumizi ya Matumizi ya Internet.

Ikumbukwe jana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa shahada ya heshima ya Falsafa ya Udaktari na chuo kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliofanyika New Delhi nchini India na kuwa Mwanamke wa kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya heshima na chuo hicho cha India 🇮🇳 .

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Manchester City face long-awaited hearing over alleged...
It has been a long wait, but the independent hearing...
Read more
TEUZI ZA RAIS SAMIA SULUHU HIVI LEO
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo...
Read more
SoccerTen Hag laments draw after United smother...
LONDON, - Manchester United manager Erik ten Hag was pleased...
Read more
Padri wa Kanisa Katoliki Mbaroni Kwa Wizi
Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda mkoani Mara hapa...
Read more
MANENO 5 AMBAYO YANASHAWISHI KILA MWANAMKE KUINGIA...
MAPENZI
Kuwepo kwa mitandao ya kijamii kumesaidia na pia kuharibu...
Read more

Leave a Reply