Kwenye maisha kuna siri nyingi basi leo nakupa siri kuhusu Mwanamke ambaye halali au kukaa kwao kama wengine.
1.MWENYE MSIMAMO
Wanawake wa daraja la kwanza wanaopendwa na wanaume ni wale wenye misimamo,uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao ya kila siku na siku zote hufanya mambo hili kufanikiwa.
2. MPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia,walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza familia 50 kwa 50.
3. ANAEJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza kwenye tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume wanapenda sana wanawake watundu kwenye mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanakuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali hisia za ndani au nje.
4.RAFIKI
Wanawake wenye sifa ya kuwa rafiki ni aina nyingine ambayo inavutia sana wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya ushawishi unaotokana na namna ya kujali na kujitolea na kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi,waungwana na wapenda amani muda wote.
5.MUWAZI
Aina nyingine ya wanawake pendwa kwa wanaume ni pamoja Mwanamke muwazi. Si wepesi wa kuburuzwa kwenye mambo ya msingi na kuwa na kisingizio cha kusema eti mimi au sisi ni wanawake. Tafiti zinaonyesha, Aina hii ya wanawake ni thabiti au kiboko kwa aina fulani ya wanaume wenye ghiliba.
6.ANAEJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na hakina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha wanaume wa kileo hawataki wanawake tegemezi, wasiopenda kazi na kuendekeza starehe tu za upande mmoja.
Nikisema wanawake wasio na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Hawa siku zote uacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.