NYOTA WETU
Muigizaji na mtangazaji Jada Pinkett Smith ameweka wazi kuwa yeye na mme wake Will Smith wametengana toka mwaka 2016 ingawa wawili hao wamekuwa wakiishi maisha ya tofauti kabisa kwa miaka saba na hawakuwa tayari kudhibitisha hilo.
Katika mahojiano yake na kituo cha NBC , Jada amekiri wazi kuwa yeye na mumewe bado wanaishi maisha tofauti, lakini hawana mpango wa kupeana talaka.
Kulikuwa na uvumi wa ndoa yao mwaka 2020 baada ya Jada kupitia Kwenye kipindi chake cha Red Table Talk kujadili uhusiano wake na Msanii August Alsina.
Waigizaji hao waliokutana mwaka 1994 na kuoana mwaka 1997 ,wana watoto wawili waliowazaa pamoja na Tery Smith, mtoto wa Smith aliezaa na mke wake wa kwanza.
Itakumbukwa Will Smith aliushangaza Ulimwengu baada ya kumcharaza kofi mtangazaji Chris Rock kwenye sherehe ya tuzo za Oscar 2022 baada ya mtangazaji huyo kufanya mzaha juu ya “upara” wa Jada Pinkett Smith.
Inashangaza kumuona Will Smith akighadhabika kiasi kile na kumpiga Chris Rock jukwaani licha ya kwamba yeye na mke wake huyo walitengana miaka 7 iliopita.