NYOTA WETU.
Jenerali Ulimwengu, Alizaliwa April 4 ya mwaka 1948 huko Ngara Mkoa wa Kagera,Tanzania, alisoma shule ya msingi Kamachumu ,katoke na Nyakato,Kagera na kidato cha tano alisoma Tabora kati ya mwaka 1955 hadi 1968 ,alikuwa Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Afrika Mashariki kati ya mwaka 1969 hadi 1972.
Akiwa ni mwanafunzi aliyesoma baada ya Azimio la Arusha katika elimu za mwanzo,Ulimwengu alikuwa mwanaharakati toka akiwa chuo kikuu na alikuwa miongoni mwa vijana waliochangia kwenye vuguvugu la kuleta uhuru.
Baada ya kumaliza Chuo kikuu alikuja kuwa mwanachama hai wa chama cha TANU na baadaye CCM ,hii ni kwa mujibu wa historia yake ya kisiasa hapa nchini ; Mwaka 1972 mpaka 1974 alikuwa kwenye Gazeti la serikali la Daily News ,na mwaka 1975 alikuwa kwenye ofisi za Area Mwanza ,pia mwaka 1974 hadi mwaka 1985 alikuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye Pan-African Youth Movement huko Algers.
Mwaka 1986 mpaka mwaka 1987 akawa Tawi la TANU vijana ,mwaka 1987 hadi mwaka 1989 alikuwa mwongozaji wa vijana kwenye michezo katika Wizara ya michezo na utamaduni mwaka 1989 hadi mwaka 1993 alikuwa mwanachama wa NEC (NATIONAL EXECUTIVE COMMITTEE ) ya Chama Cha Mapinduzi.
Novemba mwaka 1993 Ulimwengu alikuwa mwenyekiti wa Habari Cooperation, pamoja na wanahabari wengine, walianzisha gazeti la wiki la Kiswahili la RAI ,ambalo kwa muda mfupi lilikuja kuwa maarufu linalotoa habari pendwa zaidi,za kipelelezi ,uchambuzi na lenye habari zisizoongopa hapa nchini, Septemba mwaka 1995 na Februari mwaka 1998 ,chapisho lao jipya likatoka kwa lugha ya Kiswahili kila siku,lililoitwa Mtanzania, pia walianzisha magazeti yao mawili ya michezo kwa haya yote Ulimwengu alizidi kutoa makala yake .
Februari 12 mwaka 2002 ,Serikali iliukataa uraia wa Jenerali Ulimwengu ,mapema Februari mwaka 2001 Ulimwengu alitangazwa na Serikali kuwa sio Mtanzania. Hii ilikuja kwa mshtuko na mshangao mkubwa kwa watu wa ndani na wa nje ya nchi,kwasababu alikuwa ameshika nafasi mbalimbali ndani ya Serikali mpaka Ubunge na pia alikuwa kampeini meneja wa hayati Rais Benjamin Mkapa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995.