INDIA YAPINGA KUHARALISHA MAPENZI YA JINSIA MOJA

0:00

HABARI KUU

Mahakama kuu nchini India imekataa kuidhinisha mapenzi ya watu wa jinsia moja ikiwa hili ni pigo kwa wanaharakati wa kupigania haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ) katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu Duniani.

Jopo la majaji watano wa Mahakama hiyo limetangaza uamuzi huo hivi leo jumanne baada ya kusikiliza hoja za kesi hiyo kati ya mwezi April na Mei mwaka huu.

Jaji mkuu Dhananjaya Yeshwant Chandrachud amesema kwamba ilikuwa nje ya mamlaka ya Mahakama kuamua suala hilo na kwamba Bunge linapaswa kuandika sheria za kusimamia ndoa.

Hata hivyo, Chandrachud amesema serikali inapaswa kutoa ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa ndoa za jinsia moja ,akisema kuwa kuwanyima “faida na huduma “zinazotolewa kwa wanandoa wengine ni kuwanyima haki zao za kimsingi.

“Kumchagua mwenzi wa maisha ni sehemu muhimu ya kuchagua njia ya maisha. Huenda wengine wakauona huu kuwa uamuzi muhimu zaidi maishani mwao.

“Haki hii inaenda kwenye mzizi wa haki ya kuishi na uhuru chini ya kifungu cha 21 (cha katiba ya India)”.

Chandrachud amesema serikali inapaswa pia kuchukua hatua ili wana LGBTQ hawakabiliwi na ubaguzi ,ikiwa ni pamoja na kuanzisha simu za dharura na nyumba salama kwa wale walio katika mazingira magumu na kukomesha taratibu za matibabu ambazo zinalenga kubadili utambulisho wa kijinsia au mwelekeo wa kijinsia.

Uamuzi wa Mahakama unafuatia maombi yaliyodai kushindwa kutambua vyama vya watu wa jinsia moja kulikiuka haki za kikatiba za watu wa LGBTQ.

Serikali ya chama cha Bharatiya Janata ya India ,inayoongozwa na Waziri Mkuu Narendra Modi,ilipinga ombi hilo,ikisema kwamba suala linafaa kuachiwa bunge na kwamba rufaa hiyo iliwakilisha mtazamo wa mijini na wasomi.

See also  URUSI YAPITISHA SHERIA KUWAUA WANAOJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Nigeria’s newly acquired presidential jet has reportedly...
The luxury Airbus A330 aircraft, valued at a staggering N150...
Read more
Kalonzo Rejects Government of National Unity, Vows...
Wiper party leader Kalonzo Musyoka has expressed his opposition to...
Read more
16 IMPORTANT THINGS COUPLES SADLY STOP DOING...
SAYING I LOVE YOUIt is sad that it is difficult...
Read more
Manchester United will have to decide whether...
Eriksen is into his third year at Old Trafford, but...
Read more
Cagliari set to test injury-hit Juve's flawless...
Juventus have a perfect defensive record in Serie A with...
Read more

Leave a Reply