BENZEMA ATAJWA KWENYE UGAIDI KISA HIKI

0:00

MICHEZO

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa ,Gerald Damarnin ,anamshutumu Karim Benzema kwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Muslims Brotherhood, baada ya mchezaji huyo wa klabu ya Al-ittihad ya Saudia Arabia, kuonyesha kuunga mkono Taifa la Palestine katika mzozo wao na Israel, siku za hivi karibuni.

Benzema alitumia mtandao wake wa kijamii wa X na kuandika ujumbe uliosomeka,

Maombi yetu yawafikie wakazi wa Gaza ambao kwa mara nyingine ni waathirika wa milipuko hii yenye kukiuka ubinadamu ,ikiwaathiri hakina mama na watoto.

https://youtu.be/vkj4IuyEpnE?si=ofHzG_iX8n8TokJJ

Baada ya ujumbe huo ,Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alipokea ujumbe mwingi wa ukosoaji.

Gerald Darmanin alidai katika mahojiano yake,

“Kama sote tujuavyo ,bwana Karim Benzema ana uhusiano hatari na kundi la Muslims Brotherhood “


Vilevile,kipa wa zamani wa Israel, na klabu ya Mallorca, Dudu Aquate pia alitumia ukurasa wa X kumtusi Benzema kwa lugha tano tofauti, na kupelekea mtandao huo wa X kuzuia chapisho hilo,kutokana na kukiuka masharti ya Matumizi.

Tofauti na majanga mengi ya awali Duniani, suala hili la mgogoro wa Israel na Palestine imeigawa Dunia hasa kwenye soka,hasa pale inapotokea mchezaji kuguswa na kuamua kutoa maoni yake.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

PAUL MAKONDA AMUWEKA KITIMOTO MKURUGENZI WA JIJI...
HABARI KUU Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameiagiza...
Read more
WAYS ON HOW TO HAVE PEACE IN...
LOVE ❤ 15 WAYS ON HOW TO HAVE PEACE IN...
Read more
MWANZILISHI WA ACCESS BENKI WIGWE AFARIKI DUNIA...
HABARI KUU Mwanzilishi wa Benki ya ACCESS Duniani, Herbert Wigwe...
Read more
WIZKID REPORTEDLY BUYS NECK PIECE WORTH DOLLAR...
OUR STAR 🌟
See also  ALIOU CISSÉ KOCHA MKUU SENEGAL 2026
Afrobeat star, Wizkid has caused a buzz...
Read more
MUSUKUMA amshukia Luhaga Mpina Bungeni
Mbunge wa Geita, Joseph kasheku maarufu Musukuma amelishauri Bunge kumfanyia...
Read more

Leave a Reply